Home LOCAL MBUNGE MAVUNDE AANZISHA UJENZI WA SHULE KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA NGAYAGAE-IPALA

MBUNGE MAVUNDE AANZISHA UJENZI WA SHULE KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA NGAYAGAE-IPALA

Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la ya Ngayagaye kata ya Ipala wameanzisha ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi ili kuwapunguzia mwendo watoto wanaotembea umbali mrefu kufuata shule.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Uanzishwaji wa ujenzi wa Shule hii ni utekelezaji wa ahadi ya Mh. Mavunde aliyoitoa tarehe 21.09. 2025 wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu ambapo aliahidi kuanzisha ujenzi wa Shule hiyo na baadaye kuiomba Serikali kuunga mkono jitahada hizo.

“Ni dhamira ya serikali yetu kuona watoto wetu hawatembei umbali mrefu kufuata shule ndio maana leo tupo hapa kuanzisha ujenzi wa darasa la awali ili tuwapunguzie mwendo watoto wetu.

Serikali chini ya Rais Dkt. Samia S. Hassan imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa na ninaamini hata hapa itatuunga mkono juhudi hizi za wananchi.

Tutahakikisha ujenzj huu unachukua muda mfupi kukamilika kwa madarasa ili watoto hawa wapate elimu yao hapa hapa” Alisema Mavunde

Aidha wakati huo huo Mbunge Mbunge amekabidhi Matofali 2000,saruji mifuko 50,Baiskeli 20 na Bajaj kubwa mbili zenye uwezo wa kubeba watoto 20 ambazo zitasaidia usafiri wa watoto hao mpaka madarasa yatakapokamilika.

Wakitoa shukrani zao Madiwani wa Kata za Ipala na Hombolo Makulu Mh. Andrea Muhulo na Mh. Mokiwa Sahali wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa kutimiza ahadi yake ya uanzishwaji wa ujenzi wa shule na hivyo kuwataka wananchi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitahidi za Mbunge katika kufanikisha ujenzi huo.