Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI WA JENGO LA OFISI YA...

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MAENDELEO YA UKARABATI WA JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi, kuhusu maendeleo ya ukarabati wa Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli, Posta Jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Jengo hilo leo tarehe 29 Januari 2026.

……………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi leo tarehe 29 Januari 2026, ametembelea na kukagua ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais iliyopo Mtaa wa Luthuli, Posta Jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais ambaye yupo Jijini Dar es Salaam kwa shughuli mbalimbali za kikazi amekagua maendeleo ya ukarabati pamoja na uwekaji wa vifaa na samani katika ofisi mbalimbali zilizopo katika jengo hilo. 

Baada ya ukaguzi huo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Richard Muyungi, amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba ukarabati huo umekamilika kwa asilimia mia moja na Jengo litakuwa tayari kwa matumizi kuanzia tarehe 04 Februari 2026.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

29 Januari 2026

Dar es Salaam.