
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika Zanzibar leo tarehe 25 Januari, 2026.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan.





