Home LOCAL DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI

DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro amesema Chama hicho hakijengwi katika majukwaa bali hujengwa kuanzia ngazi ya mashina na matawi huku akibainisha majukwaa hutumika zaidi kwa ajili ya kutoa hamasa.

Dk.Migiro ametoa kauli hiyo leo Januari 9,2026 alipokuwa akizungumza na viongozi wa mashina na matawi wa Wilaya za Kinondoni na Ubungo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake kwa viongozi hao.

“CCM haijengwi kwenye majukwaa bali hujengwa kuanzia ngazi ya mashina, huku akibainisha kuwa majukwaa hutumika zaidi kwa ajili ya kutoa hamasa,”amesema Dk.Migiro.

Akieleza zaidi amesema uhai na uimara wa Chama hicho unatokana na nguvu ya ngazi za mashina, akisisitiza kuwa ndiko kunakojengwa misingi halisi ya CCM.

Aidha ametoa maelekezo kwa viongozi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu vikao vya mashina ili kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi na kuimarisha uhusiano wao na wananchi.

“Mashina ndiyo moyo wa CCM kwa kuwa ndiyo yanayokutanisha Chama na wananchi moja kwa moja kupitia vikao na shughuli mbalimbali za kijamii na kisiasa,amesisitiza Dk.Migiro anayendelea na ziara yake Dar es Salaam yenye kauli mbiu Shina lako linakuita.

Ameongeza “Vikao vya mashina vina mchango mkubwa katika kuyakomaza mashina, ambayo hatimaye hukua na kuwa mti imara — Chama Cha Mapinduzi.

Mwisho