
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amewasili wilayani Karagwe mkoani Kagera kumuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mwigulu Nchemba katika Ibada ya Ubarikio wa Wachungaji na Wadiakonia,tukio ambalo litafanyika kesho tarehe 21 Disemba,2025 katika Kanisa Kuu la Lukajange Dayosisi ya Karagwe.
Waziri Simbachawene amepokelewa na Askofu Dkt.Benson Kalikawe Bagonza ambae ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wilayani Karagwe ambapo jumla ya Mashemasi watano watapata uchungaji.





