Home LOCAL TUTAENDELEA KUILINDA NCHI YETU, USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO WAKATI...

TUTAENDELEA KUILINDA NCHI YETU, USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO WAKATI WOTE

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Mwandishi Wetu,  DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali yake itaendelea kuhakikisha amani, utulivu na mshikamano uliopo kwa watanzania vinalindwa kikamilifu, na kuifanya nchi kuwa salama wakati wote.

Rais Samia ametoa kauli hiyo alipozungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, kwenye mkutano uliofanyika leo Disemba 2, 2025 katika kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere JNICC, Jijini humo.

Rais Samia ametumia mkutano huo kueleza kwa kina vurugu zilizotokea wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29, nakupelekea kuwepo kwa mitazamo tofauti licha ya uwepo wa maoni ya baadhi ya watu, jinsi serikali ilivyo shugulikia tatizo hilo.

Amesema yapo maoni yaliyosema kuwa nguvu zilizotumika kwenye kudhibiti vurugu hizo ilikuwa ni kubwa, huku akihoji nguvu ndogo ambayo ingeweza kutumika ni ipi, nakwamba Dola haipo tayari kuacha baadhi ya vikundi vya watu kufanya vurugu na kuhatarisha amani.

Rais Dkt. Samia amesema serikali ya awamu ya sita anayoiongoza itahakikisha inailinda nchi na raia wake, pamoja na mali zao kwa nguvu zote.

“Serikali ina wajibu, tunaapa kuilinda nchi hii, kulinda usalama wa raia na mali zake, na katika hali hiyo nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo,”

“Sasa tunapoambiwa kwamba tulitumia nguvu kubwa sana kwenye tukio lile, nguvu ndogo ilikuwa ni ipi? ilikuwa tuwaangalie waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi na vurugu mpaka wafanikiwe?” alihoji Rais Samia.

Ameongeza kuwa Dola haipo hivyo, nakwamba mambo kama hayo hayatokei Tanzania pekee, bali kwenye nchi nyingi zikiwemo za jirani.

“Tulishashuhudia kwa wenzetu waandamanaji wengi wanaingia njiani na serikali ikiona huu uandamanaji unaenda pasipo inaweka nguvu kubwa ili kudhibiti.

“Wanapolamu kuwa tulitumia nguvu kubwa, wao walitaka nini? tujiulize, je! hao ndio wafadhili wa kile kichofanyika ?

“Walitaka wafanikiwe waliowapa fedha, walichowatuma..hapana, tuliapa kuilinda nchi hii na mipaka yake, usalama wa raia na mali zao” ameongeza Dkt. Samia