
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, utamaduni sanaa na Michezo Ndug; Gerson Msingwa amesemaSerikali kwa kushirikiana na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania
(TFF) wameakikisha timu ya Taifa ya Tanzania inapata Kila kitu kuhakikisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa start “kujianda vema huku tukitarajia kuvunja rekodi iliyopita ya kupata alama moja kwenye kundi.
Msingwa amezungumza hayo wakati kikosi cha Timu ya Taifa ikijianda kuanza safari kutoka nchini Misri kuelekea nchini Morocco ambapo ndipo mashindano ya Fainali za AFCON 2025 zitaenda kuchezwa kwanzia Desemba 21.
Hata hivyo Msingwa amesema mashindano haya yatakuwa na ujumbe maalumu ambao utawaongoza Watanzania kwenye mashindano haya ambayo yatakuwa ya mwisho kabla ya Tanzania kuanda Fainali hizo zaMataifa ya Afrika.
Tanzania itashuka dimbani Decemba 23, 2025 dhidi ya Timu ya Taifa ya Nigeria.





