Home INTERNATIONAL NAIBU WAZIRI MAGHEMBE ASHIRIKI MAADH8ISHO YA MIAKA 61 Ya UHURU WA ZAMBIA

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE ASHIRIKI MAADH8ISHO YA MIAKA 61 Ya UHURU WA ZAMBIA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe ameshiriki sherehe ya maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Jamhuri ya Zambia, zilizofanyika jijini Dar es Salaam Desemba 19, 2025.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Maghembe aliwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na aliitakia heri na mafanikio Jamhuri ya Zambia na wananchi wake.

Mhe. Magembe amesema maadhimisho ya uhuru wa Zambia, yenye kauli mbiu isemayo “Kujenga Zambia Imara na yenye Ustawi” inazikumbusha nchi nyingi za Afrika, kuhusu jitihada madhubuti zilichukuliwa na Zambia wakati wa kupigania uhuru na kuleta maendeleo ya Taifa na Wananchi wake.

Amesema jitihada za Waasisi wa Uhuru Barani Afrika akiwemo aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zambia Hayati Keneth Kaunda na Hayati Mwalimu Julius Nyerere zimeimarisha uhusiano wa uwili kati ya mataifa hayo na kuweka misingi ya amani na umoja kwa manufaa ya wananchi wao.

Mhe. Magembe ameishukuru Zambia kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia reli ya TAZARA, biashara na uwekezaji ambavyo alieleza kuwa ni utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kati ya mataifa hayo.

Awali, Balozi wa Zambia nchini Mhe. Matthews Jere alielezea azma ya nchi yake kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na Tanzania katika sekta za elimu, usafirishaji, kilimo, madini na nishati.