
.Vijana wa Kitanzania maarifu Gen Z, wameshauriwa kuzingatia misingi ya Amani, na utulivu, sambamba na kutii sheria za nchi katika kuelekea maadhimisho ya uhuru wa Tanganyika Desemba 9 mwaka huu.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 3,2025 Jijini Dar es Salaam.
Msama amesema kuwa Vijana wana wajibu wa kutambua kuwa ni nguzo muhimu katika taifa, nakwamba wasikubali kutumika na watu wenye nia ovu na nchi yao, badala yake wanapaswa kuwa wakwanza kuilinda amani iliyopo.
Aidha, amesema wazazi wana wajibu wa kuwakanya watoto wao na kuhakikisha hawakumbwi na misukumo isiyokuwa na tija
Katika hatua nyingine, amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu ya kutetea amani na vijana kusikiliza maelekezo yao.
Ameongeza kuwa hata wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanapaswa kuendelea kuhimiza vijana kuheshimu sheria za nchi, kwani hakuna haki inayoweza kutetewa nje ya misingi ya sheria na amani.




