Home BUSINESS KUTOKA UHURU HADI SASA NHC MSINGI WA MAGEUZI YA MAKAZI BORA

KUTOKA UHURU HADI SASA NHC MSINGI WA MAGEUZI YA MAKAZI BORA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

-Miradi ya kimkakati ya Awamu ya Sita yadhibitisha nafasi ya NHC kama injini ya maendeleo

Mwandishi Wetu

Tanganyika au Tanzania Bara ilipata Uhuru wake Desemba 9, mwaka 1961 na leo Desemba 9, 2025 inatimiza miaka 64 ya Uhuru wake.

Ilipata Uhuru wake kutoka kwa Waingareza, ikihitimisha enzi za ukoloni, ambapo taifa lilitawaliwa na wageni hao, ambao walikabidhiwa dhamana na Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, wakoloni hao waliondoka nchini bila kuacha mpango mkakati wowote wa makazi bora kwa wananchi wa Tanganyika huru.

Lakini kwa hekima na busara, pia kwa kutambua mahitaji ya makazi bora kwa wananchi wake, mwaka mmoja baada Uhuru, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeiongoza Serikali ya Tanganyika huru(Tanzania Bara) alianzisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), mwaka1962 kwa Sheria ya Bunge Na. 45.

Tangu wakati huo, hadi sasa Tanganyika inapoadhimisha miaka 64 ya Uhuru, Shirika la Nyumba la Taifa limeendelea kuadhimisha siku hiyo kwa kuendelea kubeba jukumu muhimu ililonalo kisheria la kuleta mageuzi ya kipekee katika sekta ya nyumba nchini. NHC ina ndoto inayoendelea kuitimiza katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata makazi bora.

  

Upo ushahidi wa wazi wa NHC kubeba jukumu hilo kikamilifu, nao ni mageuzi katika sekta ya nyumba nchini kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati ya shirika hilo linalotajwa kuwa kubwa zaidi barani Afrika, likiwa na  mtaji unaokadiriwa kufikia Shilingi Trilioni 5.

Mageuzi hayo yanaonekana wazi wazi nchini yakigusa na kushirikisha watu binafsi, Serikali, mashirika ya umma na binafsi, taasisi za fedha hata wabia.

Awamu ya Sita

Kwa kuanzia, ushahidi wa NHC iliyo bora zaidi ikibeba majukumu yake kwa ukamilifu, unapatikana kwenye kipindi hiki cha utawala wa Awamu ya Sita ambao sasa umeanza kipindi cha pili cha utawala wake, chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na hata miaka ya nyuma awamu zilizotangulia.

Hilo haliwezi kufichika kama wasemavyo waswahili; ‘Pembe la ng’ombe halifichiki’ kwani ndani ya kipindi hicho NHC limetekeleza na linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ukandarasi.

Miradi hiyo moja kwa moja inagusa na kuchangia maendeleo ya taifa Tanzania, mtu mmoja mmoja, wizara hata mashirika na kampuni.

Katika kipindi cha Awamu ya Sita pekee yaani mwaka 2023/24, hadi Disemba 2025, miradi mbalimbali imetekelezwa kama ifuatavyo:-

National Housing Corporation | Majengo ya ghorofa ya mradi wa Seven Eleven ( 711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo umerejea rasmi kwa mkandarasi... | Instagram

Ujenzi wa Jengo la Kitengo cha Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 jijini Dar es Salaam umekamilika kwa asilimia 100.

Ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Wizara nane (8) za Serikali ya Tanzania yenye thamani ya shilingi bilioni 194 katika Mji wa Serikali Mtumba.

Kuna ujenzi wa jengo la Tanzanite ulio na thamani ya shilingi bilioni 5.5 katika mji wa Mererani mkoani Manyara, ambao unaendelea kukamilishwa. 

NHC pia inatekeleza ujenzi wa Jengo la Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wenye thamani ya Shilingi Bilioni 9.8.

National Housing Corporation | Majengo ya ghorofa ya mradi wa Seven Eleven ( 711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo umerejea rasmi kwa mkandarasi... | Instagram

 Si hivyo tu bali inatekeleza pia ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambao hivi karibuni Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi alitembelea na kukagua.

NHC ikitekeleza pia mradi wa jengo la Wizara ya    Fedha, ujenzi wa Hospitali za Kanda ya Kusini (Mitengo) na Kanda ya Ziwa (Mwalimu Nyerere). 

Ifahamike kuwa utekelezaji miradi hiyo hata mingi mingine iliyopo, isingewezekana bila NHC kufanyiwa mageuzi na kuiwekea mpango mkakati ikitazamwa historia yake na malengo yake katika sekta ya nyumba.

Mkakati wa Maendeleo NHC

Kwa kuangalia mambo hayo mawili pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo, Mwaka 2010 na sasa Dira ya Taifa ya 2025-2050, Serikali ilianza awamu mpya ya kuimarisha NHC kwa kuboresha Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti. Lengo kufanya hivyo lilikuwa kuongeza ufanisi, kujenga nyumba zaidi na kufanikisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.

Katika mazingira hayo Mpango Mkakati wa Miaka 10 kuanzia mwaka 2015/16–2024 hadi 2025 uliandaliwa. Mpango huu umelenga ujenzi wa nyumba 10,000, usimamizi wa miradi mikubwa ikiwemo ya Serikali na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na taasisi za kifedha.

Mpango huo pia umetoa dira ya ukuaji wa sekta ya nyumba nchini, kwa kuweka mkazo mahitaji ya sasa, ongezeko la idadi ya watu na mustakabali wa taifa kwenye sera ya Ardhi na Makazi.

Sura ya utekelezaji

Ni machache pekee yaliyotajwa kutekelezwa katika Awamu ya Sita, lakini tangu Uhuru hadi sasa NHC imefanikiwa kutekeleza na kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo, ikiwa ni ushahidi mwingine wa mafanikio ya shirika hilo kwa kipindi chote cha uhai wake wa miaka 63, tangu lilipoanzishwa mwaka 1962, wakati huu inapoadhimishwa miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara(Tanganyika).

Miradi iliyotekelezwa na kukamika tangu Uhuru inajumuisha:

NHC WAPEWE MAUA YAO KUKAMILISHA MRADI ...

Ujenzi wa nyumba 887 za makazi za kawaida katika eneo la Iyumbu na Chamwino Mkoani Dodoma (404), Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe (50), Chartur Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga (10) na Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi (24).
Kwanza ni ujenzi wa nyumba 521 kwa ajili ya biashara katika eneo la Mtukula mkoani Kagera (45), Medeli mkoani Dodoma (42), Dar ss Salaam (380) na Mwanza (54).  

Pia kuna ujenzi wa nyumba 1,187 kwa ajili ya makazi na biashara katika eneo la Morocco Square (1,100) na miradi ya ubia (87) katika Jiji la Dar es Salaam.

NHC imeongeza rasilimali zake kwa kununua nyumba 896, zikiwemo nyumba za makazi 389 na nyumba nyingine 497 za bashara eneo la Urafiki, mkoani wa Dar es Salaam.

Mbali na miradi hiyo iliyokamilishwa, Shirika la Nyumba la Taifa, linaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi iliyo katika hatua tofauti za ujenzi.

DRONE: MOROCCO SQUARE MALL IS OPEN ...

Miradi hiyo inajumuisha; Ujenzi wa nyumba 560 katika mradi wa “Samia Housing Scheme” Awamu ya Kwanza katika eneo la Kawe jijini Dar es Salaam ambao umefikia zaidi ya asilimia 65. Mradi huu utawezesha ujenzi wa nyumba 5,000 nchini zitakazogharimu takriban shilingi bilioni 466.

Mauzo ya nyumba hizo za Kawe yanaendelea hii ikitokana na msukumo maalum wa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufungua milango ya uchumi na uwezeshaji wa mapato kwa wananchi.

Pia kuna ujenzi wa nyumba 1,533 za makazi na biashara. Katika mradi wa Kawe 711 zinajengwa nyumba (422) na umefikia asilimia 45 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili 2026. Aidha, pia kuna ujenzi wa nyumba 532 kupitia mradi wa Golden Premier Residence.

Shirika na Sekta ya Fedha

NHC katika eneo hilo limekuwa kiunganishi muhimu kati ya wananchi na taasisi za kifedha nchini, ambapo zaidi ya benki 22 zimeungana na shirika hilo likiwezesha mikopo ya nyumba ya muda mrefu kwa wananchi, huku nyumba zake zikitumika kama dhamana kwa wakopaji kupitia mikataba maalum na wateja kwake wa nyumba.

NHC na Sekta Binafsi

Kupitia sera ya ubia, NHC imefungua milango kwa sekta binafsi kushiriki katika ujenzi wa nyumba na majengo ya kisasa. Ushirikiano huo umeongeza ushindani, ubora na kupanua fursa za uwekezaji katika sekta ya nyumba nchini.

Sera ya Ubia iliyohuishwa mwaka 2022, imeiwezesha NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi ya ubi ana sasa jumla ya miradi 20 yenye thamani ya Shilingi bilioni 191 iko tatika hatua mbalimbali za ujenzi.

Kupitia mfumo huo, majengo makubwa ya kibiashara yamejengw na yanaendelea kujengwa katikati ya miji mbalimbali nchini.

Huo ni ushahidi wa mchango wa NHC katika kuboresha mandhari ya miji kwa miradi kama vile ya nyumba za makazi na ofisi, ambazo sasa ni chanzo kikuu cha ajira kwa vijana na kinamama pia maendeleo ya kiuchumi kwa taifa.

 Maono na historia ya NHC

Ikumbukwe kuwa Serikali chini ya Hayati baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ilianzisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kwa sheria ya Bunge, mwaka mmoja tu baada ya Uhuru wa Tanganyika.

Hakuna wa kubisha kwamba hiyo ilikuwa ni sehemu ya maono ya Rais wa Waziri Mkuu wa Kwanza, ambaye pia alikuw Rais wa Kwanza wa Tanganyika, Mwalimu Nyerere, kuhakikisha mahitaji ya msingi ya mwanadamu kama makazi, chakula na mavazi yanapatikana kwa kila mwananchi.

Shirika la Nyumba la Taifa katika miaka ya mwanzo majukumu yake yalitekelezwa kupitia miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba na majengo ya umma, lakini utendaji wake uliathiriwa na hangamoto za kiuchumi na kisheria.

Moja ya sheria zilizosababisha NHC na sekta ya nyumba nchini kusuasua ilikuwa Sheria ya Zuio la Kodi ya Mwaka 1984 ambayo ilizuia uwekezaji wa sekta binafsi, iliyokuwa pia  na masharti magumu kwa wamiliki wa nyumba.

Hata hivyo mwaka 1990 mageuzi yalifanyika, ambapo NHC liliunganishwa nailiyokuwa Msajili wa Majumba. Hili lilifanyika kupitia Sheria Na. 2, na NHC likapewa mamlaka mapya ya kusimamia nyumba zilizotwaliwa na Serikali mwaka 1971.

Ikumbukwe kuwa mwaka 2005 Bunge lilifanya hatua muhimu, ambapo lilifuta sheria ambazo hazikuwa rafiki kwa NHC na uendeshaji wake, kisha kuweka mazingira bora kwa uwekezaji. Katika mabadiliko hayo muhimu, Bunge liliziboresha Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 na Sheria Na. 2 ya mwaka 1990, ambazo ziliunda upya Shirika la Nyumba la Taifa.

Sasa na baadae

Shirika linaendelea kupanua wigo wa shughuli zake kwa kutumia utaalamu na wataalam wa ndani hasa vijana na teknolojia ya kisasa.

Lengo la NHC katika hayo ni kuimarisha utendaji kazi wake,kutoa huduma bora kwa wananchi, likiongeza ufanisi wa miradi na kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi za Serikali na gawio.

Katika miaka ijayo, NHC ina mpango wa kuanzisha miradi mingi zaidi ya makazi, kuimarisha uhusiano wa kimataifa, pia kutoa ushauri wa kitaalamu katika miradi mbalimbali.

Moja ya mambo muhimu ya kukumbukwa ya NHC katika miak 64 ya Uhuru wa Tanganyika ni shirika hilo kushiriki katika kuasisi Shirika la Nyimba Zanzibar (ZHC), mwaka 2014.

inocomm.blogspot.com: MKURUGENZI MKUU WA NHC ATEMBELEA MIRADI GEITA NA MWANZA

Si hivyo tu, bali limeendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa ZHC ya namna Shirika la Nyumba linavyotakiwa kujiendesha, likiendelea kushirikiana nalo katika kuimarisha maendeleo ya nyumba ukanda wa Afrika Mashariki. 

Mapema, NHC ilitoa mafunzo ya kitaalam na kwa wataalam wa ZHC ambapo walijifunza mambo ya nyumba, ikiwemo kuhusu utayarishaji wa Sheria za Shirika la Nyumba Zanzibar. 

Kati ya NHC na ZHC zimefanyika ziara mbalimbali za kubadilishana uzoefu zikigusa Bodi na Menejimenti za pande mbili za Muungano.

Tangu kuanzishwa kwake wa zaidi ya miaka 63, NHC linabaki kuwa kiungo muhimu kwa safari ya Tanzania kuelekea makazi bora kwa kila mwananchi. 

NHC linaonyesha mfano wa jinsi taasisi za umma nchini, chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, zinavyoweza kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kupitia mipango madhubuti, NHC imeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya sekta ya nyumba likihakikisha kila mwananchi anashirikishwa katiika haki ya kupata makazi bora na kufurahia huduma bora za shirika.