
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.Asha-Rose Migiro ameshiriki mkutano wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), leo Jumanne,Desemba 2,2025 Jijini Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo maalum,mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan.





