Home LOCAL HADI KUFIKIA MCHANA HUU HALI NI SHAWARI

HADI KUFIKIA MCHANA HUU HALI NI SHAWARI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini DCP David Misime amesema kuwa mpaka mchana wa leo Disemba 9 hali ya usalama ni shwari katika maeneo yote nchini nzima.

Misime ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha usalama wa watu na mali zao, sambamba na kuhakikisha amani inatawala nchini.

Aidha, Polisi imewataka wananchi kupuuza picha mnato na picha mjongeo zinazoenezwa mitandaoni zikidai kuwa maandamano yameanza sehemu mbalimbali za nchi, akibainisha kuwa picha hizo ni za matukio ya zamani zikiwemo zile za Oktoba 29, 30 na 31, 2025.

Misime ameyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari, kuhusu hali ya usalama wa nchi kwa ujumla,

ikiwa ni siku maalum ya maadhimisho wa Uhuru wa Tanzania Bara, inayoadhimishwa Desemba 9, kila mwaka. Aidha, taarifa hiyo imetolewa kufuatia tishio la uwepo wa maandamano yasiyo na kikomo, nakwamba maandamano hayo siyo rasmi na kupigwa marufuku na Jeshi hilo.