Home LOCAL DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA BANDARI YA UVUVI, KILWA.

DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA BANDARI YA UVUVI, KILWA.

http://DKT. MWIGULU AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA BANDARI YA UVUVI, KILWA.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

_Asema Rais Dkt. Samia ni kiongozi anayetekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania_.

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi huo, Dkt. Mwigulu amesema kuwa bandari hiyo ni mojawapo ya miradi mingi inayofafanua kauli za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alizozitoa baada ya kuapishwa za kusimamia utekelezaji wa miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kubadili maisha ya Mtanzania pamoja na kuongeza pato la Taifa. “Rais Dkt. Samia ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za watanzania”

Ameongeza kuwa ili kuhakikisha mradi huo unafanya vizuri Rais Dkt. Samia ameahidi kununua meli 5 za uvuvi. “Tanzania inakwenda kuandika historia mpya kwenye sekta ya uvuvi, Rais Dkt. Samia aliahidi kuendeleza miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake na mmoja wapo ni wa Bandari ya Uvuvi iliyopo wilayani Kilwa.”

Mradi huo ambao umefikia asilimia 90 ya ujenzi wake umegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 280.