Home BUSINESS BENKI YA ABSA YASHINDA TUZO YA ‘BENKI INAYOPENDEKEZWA NA KUFIKIWA ZAIDI MASHARIKI...

BENKI YA ABSA YASHINDA TUZO YA ‘BENKI INAYOPENDEKEZWA NA KUFIKIWA ZAIDI MASHARIKI NA KUSINI MWA AFRIKA’

Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Mwilongo (katikati), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake, wakionesha tuzo ya ‘Benki Inayopendekezwa na Kufikiwa zaidi Mashariki na Kusini mwa Afrika’ mara baada ya kukabidhiwa, katika hafla ya utoaji wa tuzo za Chaguo la Walaji Afrika 2025, jijini Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania Bi. Irene Mwilongo (wa tatu kulia), akipokea tuzo ya ‘Benki Inayopendekezwa na Kufikiwa zaidi Mashariki na Kusini mwa Afrika’ kutoka kwa Mwakilishi kutoka waandaaji wa tuzo hizo, Bi. Balqis Njuki, katika hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji Afrika 2025, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkuu wa Uchambuzi wa Utendaji wa Biashara wa Benki ya Absa Tanzani, Bw. Stivia Augustino (wa tatu kulia), akionesha tuzo ya ‘Benki Inayopendekezwa na Kufikiwa zaidi Mashariki na Kusini mwa Afrika’, katika hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji Africa 2025, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkuu wa Mikakati na Data wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. John Mosha (wa nne kulia), akizungumza baada ya kupokea tuzo ya ‘Benki Inayopendekezwa na Kufikiwa zaidi Mashariki na Kusini mwa Afrika’, katika hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji Africa 2025, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.