
Wenyeji wa mchezo wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara, (NBC), JKT Tanzania, ilijikuta katika wakati mgimu kwa kuchezea kichapo cha magoli 2-1, dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba SC, katika mtanange uliopigwa Novemba 8 katika Dimba la Meja Jeneral Isamuyo Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mwenyeji JKT Tanzania walitangulia kupata bao la uongozi katika dakika ya 45 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.
Timu ya Simba ilionesha makucha yake mithili ya mnyama aliyejeruhiwa, ambapo Edward Songo aliifungia timu hiyo goli la kusawazisha katika dakika ya 60 ya mchezo huo.
Mshambuliaji wa Simba Jonathan Sowah ilipigilia msumari wa pili akiifanya Simba kumaliza dakika 90 na alama tatu muhimu, na kuiwezesha timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa alama 9 baada ya kushinda mechi tatu mfululizo .





