Home LOCAL SERIKALI YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI VYA NJE KUACHA UPOTOSHAJI

SERIKALI YAVITAKA VYOMBO VYA HABARI VYA NJE KUACHA UPOTOSHAJI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Serikali imevitaka vyombo habari vya kimataifa vinavyoripoti kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini, ikivituhumu kuchapisha taarifa za upande mmoja na zinazoweza kuchochea chuki miongoni mwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Gerson Msigwa, alisema kuwa kumekuwa na wimbi la upotoshaji unaofanywa na baadhi ya media za nje ambao umesababisha madhara makubwa katika jamii.

Msigwa alisema wakati taifa likisubiri tume maalumu kukamilisha uchunguzi wake, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikichapisha taarifa zinazolenga kuchochea chuki, migawanyiko ya kisiasa, kidini na kikanda.