
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-
Bw. Tido Mhando ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, Habari na Mawasiliano;
Bw. Bakari Steven Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu.
Bw. Machumu anachukua nafasi ya Bi. Sharifa Bakari Nyanga ambaye amepangiwa majukumu mengine;
na Bw. Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa kuwa Balozi.
Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Bkt. Moses M. Kusiluka,
KATÍBU MKUU KIONGOZI
19 Novemba, 2025




