Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi kuwa Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika cheo cha Luteni Usu kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 22 Novemba, 2025.





