Home LOCAL ZITTO: CCM HAIWEZI KUONDOKA MADARAKANI BILA UCHAGUZI

ZITTO: CCM HAIWEZI KUONDOKA MADARAKANI BILA UCHAGUZI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Ikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema njia pekee itakayoweza kukiondoa chama cha CCM madarakani ni wananchi kukikataa chama hicho kupitia sanduku la kura.

Akizungumza leo, Oktoba 14, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Mirongo jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Kiongozi mstaafu wa chama hicho, Zitto Kabwe amesema kulingana na historia na hali ya nchi kisiasa haiwezekani kuiondoa serikali iliyopo madarakani bila mchakato wa uchaguzi

Alifafanua kuwa itikadi ya chama cha CCM ni kushika madaraka hivyo chama hicho hakijali uamuzi wa chama kingine kususia mchakato wa uchaguzi.

“Najua watu wamekatishwa tamaa na mambo yaliyotokea 2020, 2024 wanaona kura zao hazina thamani tena, hata wakipiga kura wanaotangazwa sio waliowachagua”, alisema Zitto

Hata hivyo, Zitto alisema viongozi wa dini hawajawahi kuchoka kuhubiri kuhusu uovu licha ya maovu kuendelea kuwepo katika jamii yetu, hivyo wananchi hawapaswi kukata tamaa na kuwasusia CCM mchakato wa uchaguzi.

Naye mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Esther Thomas aliahidi kuboresha sekta ya elimu katika jimbo hilo kwa kuhakikisha anajenga maktaba za kisasa kwa kila kata katika jimbo hilo.

Pia aliahidi kuboresha hudumq ya usafiri kwa ajili ya wanafunzi ambapo atatafuta usafiri wa gharama nafuu utakaokuwa unajiendesha wenyewe.