Dar es Salaam.
1.Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linapenda kuutarifu umma kuwa wapo baadhi ya waliokuwa wapangaji wa nyumba za NHC ambao waliondoka kinyemela kwenye nyumba za Shirika na kuacha madeni ya kodi za pango.
2.Tunawakumbusha waliokuwa wapangaji na kuacha madeni ya pango, kuhakikisha kuwa wanalipa madeni yao yote ya kodi ifikapo Oktoba 15, 2025.
3.Ni wajibu wa kisheria na kimkataba kwa kila mpangaji wa nyumba za NHC kulipa kodi yake kikamilifu.
Hivyo, mdaiwa yeyote atakayeshindwa kulipa madeni yake ifikapo tarehe tajwa, atachukuliwa hatua za kisheria pamoja na:-
- Kutangazwa hadharani kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijami
- Kufikishwa kwa madalali waliosajiliwa na mahakama walioteuliwa na Shirika kukusanya madeni,
- Kupelekwa majina yao kwenye “Credit Information Bureau (CIB)” ili kunyimwa fursa za mikopo katika taasisi za fedha.
4.Kwa utaratibu wa marejesho ya madeni, wadaiwa wote wanahimizwa kuwasiliana na Mameneja wa Mikoa husika, ili kuandaa mpango wa malipo na kuepuka usumbufu mkubwa unaoweza kujitokeza.
5.NHC haitavumilia vitendo vya kukwepa wajibu wa kulipa kodi. Ni wajibu wa kila mdaiwa kutekeleza wajibu wake kwa wakati.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA