
“Nataka kuwahakikishia Vijana wa Kitanzania msidanganywe, ukichukua Afrika Mashariki pengine na kusini na Kati mwa Afrika, Tanzania ni pepo. Hapa upo kwenye nchi yenye jina, yenye sifa zake na yenye kuendeleza watu wake. Msidanganywe na wale walioko huko nje, hapa mpo pazuri kwelikweli. Ukipata fursa tu za kuingia kwa majirani zetu hapo kaangalie Vijana wenzenu wanavyokula ngumu, unaweza ukasema mimi narudi Tanzania, Tanzania ndiyo kwetu.
“Kwahiyo niwaambie Vijana sisi wazazi wenu tunapita, nchi hii inawategemea ninyi, tunatarajia tuwaachie nchi muiendeshe kama tunavyoiendesha sisi, kwahiyo Vijana wa Tanzania msidanganywe hata kidogo. Hakuna maeneo mengine wanangu, tulizeni munkari, kaeni vizuri hii nchi ni mali yenu si ya mwingine na hakuna mwenye cheti cha kusema hii nchi yangu.
…. Niwaombe msiharibu amani ya nchi yenu, fuateni serikali yenu inavyowaelekeza, fuateni Katiba yenu inavyowaelekeza, fuateni sheria za nchi zinavyotaka, mtaishi kwa salama, kwa amani wala hamtasumbuliwa.”- Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, akizungumza kwenye Kampeni zake Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam leo Alhamisi Oktoba 23, 2025.





