
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Kusini na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Ndugu. Aden Mayala amekihama na kuachana kabisa na chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ndugu. Mayala amepokelewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo tarehe 22 Oktoba 2025 wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. uliofanyika viwanja vya Kecha Ilala Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kupewa fursa ya kutoa salamu katika mkutano wa kampeni za Dkt. Samia, Kinyerezi Ilala, Dar es salaam leo Oktoba 22, 2025, Mayalla ametaja sababu nyingine ya kutimkia CCM kuwa ni kitendo cha Dkt. Samia kuahidi kwamba akichaguliwa Oktoba 29, atahakikisha mchakato mpya wa katiba utaanza.
.heic)
Mayalla ambaye pia alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, ametaja sababu zilimfanya akihame kuwa ni uwepo wa unyanyasaji na ubaguzi uliokithili kati ya kambi za walioshinda na walioshindwa katika chaguzi zao, chama hicho kutokuwa na Future, ajenda ya kutoshiriki uchaguzi mkuu na kutokukubaliana na kitendo cha kuandamana kupinga uchaguzi mkuu Oktoba 29.
Ametoa wito kwa Watanzania kuachana na upuuzi huo wa kuandamana bali washiriki ipasavyo katika Uchaguzi Mkuu na kuhakikisha wanampigia kura za kishindo Mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Samia kwa vile ana uwezo mkubwa, ameupiga mwingi katika kuliletea Taifa Maendeleo ya dhati.
.heic)




