Home LOCAL TEF YALAANI KAULI ZA KULIINGIZA JESHI KWENYE SIASA

TEF YALAANI KAULI ZA KULIINGIZA JESHI KWENYE SIASA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

OKTOBA 4, 2025, mitandao ya kijamii ilisambaza picha na video zikionesha watu wawil wanaodai kuwa wanajeshi, wakihamasisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiingiza kwenye siasa kwa njia ya mapinduzi. Pia kwa muda sasa kuna watu wanaojiita wanaharakati vanaosambaza matusi dhidi ya viongozi wa nchi mitandaoni, badala ya ajenda au sera.

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) linapongeza hatua ya haraka ya JWTZ kutoa taarifa kwa umma kukemea matendo hayo ndani ya muda mfupi Taarifa ya JWTZ inasema: “JWTZ inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania, kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni wa saba tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Ni kawaida kuona joto la kisiasa na mijadala mikali ya sera nyakati za uchaguzi, lakini si hoja za kupinduana. Tunashuhudia nchi zilizofanya mapinduzi jinsi watu wao wanavyoishi kwa mateso, umwagaji damu, uharibifu wa mali na kudhoofisha taasisi za nchi.

Tanzania ilijaribiwa mapinduzi mwaka 1964, 1969- na 1982, lakini H kwa hekima, ya viongozi na umoja wa Wananchi, nchi yetu ilishinda majaribu hayo na kujenga mfumo thabiti unaotenganisha Jeshi na siasa. Wanajeshi wa Tanzania hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya sıasa msingi huu ndiyo ngao ya amani na utulivu wetu.

Kauli za kujaribu kuchochea Jeshi uasi ni hatari, zinavunja misingi ya Taifa na kuharibu mwelekeo wa taifa lolote duniani. TEF inaasa vyama vya siasa visijihusishe kwa namna yoyote na fikra za mapinduzi kama njia ya mkato kuingia madarakani, bali vijijenge kiushindani kisera, vikiamini katika nguvu ya sanduku la kura.

TEF tunatoa angalizo maalumu kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii. Tumeshuhudia nitandao ikitumika kusambaza taarifa zisizo sahihi, picha na video zenye upotoshaji na matusi zinazoweza kuhatarisha amani ya Taifa letu. Tunasihi Watanzania kuwa makini na kuchunguza ukweli kabla ya kusambaza taarifa kwenye simu Wenye mitandao watangulize maadili, uzalendo na uwajibikaji, badala ya kugeuza majuk waa hayo kuwa vyanzo vya hofu na chuki.

Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu.

Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amanı, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi.

TEF tunakemea kauli za kuhamasisha mapinduzi, tunaipongeza JWTZ kwa uaminifu wake kwa Katiba, na tunasihi Watanzania wote kulinda amani na umoja wa Taifa letu, muda wote.

Mungu Ibariki Tanzania
JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)

Deodatus Balile

Mwenyekiti 

05/10/2025