
Timu ya Soka ya Singida Big Stars imefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho Brani Afrika, kwa kuirarua timu ya Frambeau Fc jumla ya magoli 3-1, katika mtanange uliopigwa kwenye Dimba la Azam Complex, Jijini Dar es es Salaam.
Katika mchezo huo ulichezwa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Mashariki, timu ya Frambeau FC. ndio ilitangulia kutikisa nyavu za Singida, goli lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Singida BS, wakionekana kuutaka mchezo huo, ambapo nyota mzambia Clatus Chama aliipatia tiu yake goli la kusawazisha, akifunga kwa mkwaju wa penati, na kufungua ukurasa wa Masoli kwa Singida Big Stars.




