Home BUSINESS MIAKA 26 KIFO CHA MWL. NYERERE, NHC YAFANIKISHA NDOTO MAKAZI BORA NCHINI

MIAKA 26 KIFO CHA MWL. NYERERE, NHC YAFANIKISHA NDOTO MAKAZI BORA NCHINI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

– NHC chini ya Rais Dk. Samia imefufua falsafa ya utu ya Mwalimu Nyerere

Kila inapowadia tarehe 14 Oktoba, Watanzania hukusanyika kwa heshima na kumbukizi ya maisha na kazi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, NHC limepata mwanga mpya wa ufanisi na ubunifu.

Kupitia dira yake ya uwekezaji na ubia, miradi mikubwa ya nyumba imezinduliwa, ikiwemo Samia Housing Scheme inayolenga kujenga nyumba 5,000 kote nchini.

Tayari nyumba 560 za awamu ya kwanza Kawe zimekamilika na zote kuuzwa hata kabla ya ujenzi kukamilika, hii ni ishara ya uhitaji mkubwa na imani ya wananchi kwa NHC.

Sambamba na ujenzi wa nyumba za makazi na biashara, NHC chini ya Serikali inayoongozwa na Rais Sami, limekuwa mshauri na msimamizi wa miradi mbalimbali ya kitaifa.

Hii ni pamoja na ukarabati na ujenzi upya wa Soko la Kariakoo ambalo limeshakamilika, Jengo la Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa asilimia 95, Jengo la Makamu wa Rais – Mazingira kwa asilimia 90 na Soko la Madini la Tanzanite Mirerani kwa asilimia 100.

Katika uendelezaji wa sera ya ubia, NHC liliboresha sera yake mwaka 2022, likiunga mkono sera ya ufunguaji uwekezaji iliyoasisiwa na Rais Samia. Hadi sasa mikataba 21 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 179 imesainiwa, na miradi kadhaa iko katika hatua mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa NHC  Bw. Ahmad Abdalla akizungumza katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miradi 21 ya ubia ya majengo ya biashara na makazi, katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam, kwakushirikiana na Sekta Binafsi, yenye thamani ya Shilingi Bilioni 271.

Katika eneo la Kariakoo pekee, nyumba 172 zilizokuwa zimevunjwa zitatekelezwa upya na kuibua zaidi ya nyumba 2,100 za kisasa za makazi na biashara.

Shirika pia limeleta mageuzi makubwa katika ujenzi wa miradi ya kibiashara na ya kijamii. Mradi wa Morocco Square jijini Dar es Salaam ni mfano hai: asilimia 100 ya nyumba za makazi zimeuzwa, maduka yote yamepangishwa, na hoteli yenye vyumba 81 sasa inatoa huduma.

Muonekano wa Mradi wa Kawe 711, Jijini dar es Salaam, ukikamilika

National Housing Corporation | Majengo ya ghorofa ya mradi wa Seven Eleven ( 711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo umerejea rasmi kwa mkandarasi... | Instagram

National Housing Corporation | Majengo ya ghorofa ya mradi wa Seven Eleven ( 711) Kawe zinavyoonekana zitakavyokamilika. Ujenzi wa mradi huo umerejea rasmi kwa mkandarasi... | Instagram

Muonekano wa Jengo la Kawe 711 llililopo kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambapo likikamilika litakuwa na sehemu ya kuishi, kufanyia kazi, pamoja na maeneo maalum ya kupumzika enye utulivu, usalama, na mandhari mazuri ya kuvutia.

Miradi mingine kama Kawe 711, Kahama Plaza, Masasi Plaza na Mtanda Commercial Building mkoani Lindi uliokamilika kwa asilimia 93, na 2H Commercial Building mkoani Morogoro uliokamilika kwa asilimia 99 yakiakisi ubora wa usimamizi wa kisasa.

Kwa upande wa ukandarasi, NHC limepewa jukumu kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya kitaifa, ikiwemo majengo ya Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba, Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hospitali ya Kanda ya Kusini – Mitengo, na Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Musoma.

Matokeo ya kazi hii yote yanaonekana wazi: mapato ya Shirika yamepanda, mali zake zimeongezeka hadi kufikia zaidi ya trilioni 5, na wananchi wengi zaidi wanapata fursa ya kumiliki nyumba kupitia mikopo ya muda mrefu inayotolewa kwa kushirikiana na benki zaidi ya 22.

Miaka 26 tangu tumuage Mwalimu Nyerere, urithi wake bado unaishi kupitia NHC. Kila jengo jipya linaloinuka, kila familia inayopokea funguo za nyumba, na kila mji unaopata sura mpya ni ishara kwamba ndoto ya Baba wa Taifa inaendelea.

Kwa hakika, NHC si tu shirika la nyumba, bali ni sehemu hai ya historia, falsafa na ndoto ya kujenga taifa lenye utu, usawa na maendeleo endelevu.

Ikumbukwe kuwa Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 katika Hospitali ya St. Thomas Jijini London

Ni siku inayobeba hisia nzito, si tu kwa sababu aliongoza harakati za ukombozi, bali pia kwa sababu alisimamia maono ya kujenga taifa lenye utu, heshima na usawa.

Miongoni mwa mambo yaliyokuwa karibu sana na moyo wake ni suala la makazi bora aliamini kwamba mtu hawezi kuishi kwa heshima bila nyumba salama na yenye hadhi.

Kutokana na falsafa hiyo, mwaka 1962 Nyerere akiwa kiongozi wa Serikali ya Tanganyika (baadaye Tanzania) alianzisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia Sheria ya Bunge Na. 45.

Lengo lilikuwa wazi, kuhakikisha kila Mtanzania anapata makazi bora.

Nyerere alisisitiza kwamba taifa changa haliwezi kusimama imara kama wananchi wake wataendelea kuishi katika makazi duni.

Hivyo, NHC likawa sehemu ya urithi wake wa kijamii, chombo cha kuendeleza utu na mshikamano wa Watanzania.

UMOJA WA KITAIFA: Somo la milele kutoka kwa Mwalimu Nyerere - HabariLeo

Miaka ikasonga, changamoto za kiuchumi na kisera zikajitokeza, lakini azma haikupotea. Kufikia miaka ya 1990, mageuzi makubwa yalifanyika, na NHC likapewa uwezo wa kujiendesha kibiashara huku likidumisha wajibu wake wa kijamii.

Mageuzi haya yakaliweka Shirika kwenye ramani kama taasisi thabiti, yenye uwezo wa kushirikiana na sekta binafsi na kutekeleza miradi mikubwa ya kitaifa.

NHC WAPEWE MAUA YAO KUKAMILISHA MRADI ...

DRONE: MOROCCO SQUARE MALL IS OPEN ...

Muonekano wa Jengo la Morocco Square llililopo kwenye makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Chole Road,Morocco Jijini Dar es Salaam, ambalo linajumuisha maduka, ofisi, migahawa na makazi.