Home LOCAL MAELFU WAMSUBIRI BARABARANI KUMLAKI DKT. SAMIA NYAMAGANA

MAELFU WAMSUBIRI BARABARANI KUMLAKI DKT. SAMIA NYAMAGANA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Maelfu ya wananchi wa Buhongwa Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza wakiwa wamejitokeza kwa wingi pembezoni mwa barabara, tayari kwaajili ya kumlaki na kumsikiliza Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Oktoba 07, 2025. Dkt. Samia amerejea kwenye Kampeni zake mara baada ya mapumziko mafupi na zamu hii akitarajiwa kurindima kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa akianza na Mkoa wa Mwanza kwenye Wilaya za Nyamagana, Misungwi pamoja na Wilaya ya Sengerema.