Home LOCAL KATIBA MPYA ITAIMARISHA UTAWALA WA SHERIA NCHINI- DKT. SAMIA

KATIBA MPYA ITAIMARISHA UTAWALA WA SHERIA NCHINI- DKT. SAMIA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza maelekezo ya Chama chake ya Kutaka Tanzania kuwa na Katiba mpya ndani ya miaka mitano ijayo, akisema suala hilo limekuwa hitaji la muda mrefu la wananchi na wanachama wa vyama vya siasa nchini ikiwemo wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

Kupitia Katiba hiyo, Dkt. Samia wakati akifunga Kampeni zake Visiwani Zanzibar leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Unguja amesema upatikanaji wa Katiba mpya ndani ya miaka mitano ijayo litasaidia katka ujenzi wa mazingira bora ya utawala bora na utawala wa sheria.

Dkt. Samia pia amesisitiza kuhusu usimamizi wa ulinzi na usalama wa nchi na raia wake, akisema wamefanikiwa kuenzi mambo hayo tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania, akiahidi kutokuwa na longolongo katika kuhakikisha kuwa nchi inabakia salama na raia wanaishi kwa amani, usalama na uhuru, akisisitiza pia kuendelea kulinda na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ili kuiweka nchi katika heshima kubwa Kimataifa kwa kulinda Uhuru, Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Heshima ya Tanzania.

Dkt. Samia kadhalika amerejea wito wake wa kuwataka wananchi wote wenye sifa na waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29, 2025 na kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM, ili kiweze kuwaongoza watanzania kwa miaka mitano ijayo na kuweza kuwaletea maendeleo.