“Mgombea wetu umetufundisha mengi na umethibitisha kwamba utu kwako ni kipaumbele na pia kazi ndiyo msingi wa maendeleo kwamba hata kama tutakaa kama Taifa tukazungumza mambo mengi tutakavyo kama hatufanyi kazi maendeleo ni ndoto na maendeleo yoyote hayawezi kutokea kama hakuna utu. Umethibitisha utu, umejenga daraja la maridhiano kwenye nchi yetu, kila mtu amesikilizwa hata walioomba Katiba mpya ukasema lisiwe jambo la kutamkwa tu, ukaliweka kwenye Ilani hii ili kwamba liwe deni kwako kwamba katika kipindi kijacho cha miaka mitano utawapatia Katiba mpya kama walivyoomba.
“Mama umetufundisha mengi, umetufundisha kuwavumilia watu, umetufundisha kuwaheshimu watu lakini pia umetufundisha kutenda zaidi badala ya kusema. Wewe ni tofauti na wengi unasema kidogo, unatenda zaidi kwamba katika kipindi chote cha Uongozi wako umekuwa mwalimu wetu wengi kwamba kazi ndiyo utakayopimwa nayo hutapimwa kwa aya utakazozisema au kughani bali utapimwa kwa maendeleo yanayotokea kwa watu tena yasiyotamkwa kwa mdomo bali yanayoonekana kwa macho.
…. Na sisi hapa hatuuchukulii uchaguzi huu poa. Tunauchukulia uchaguzi huu kama uhusiano wa maisha yetu na tutakuchagua kwasababu moja, umetupenda na ukatupendelea. Sisi hatusikilizi maneno ya watu, sisi Bukombe tunajua neno moja tu kuwa umetupendelea, Hatukuwa na soko la Kisasa, Mama Samia ametuletea soko la Kisasa. Tunajua neno moja tu tulikuwa hatuna maji, mama ameleta maji, hatukuwa na Vyuo, Mama ametuletea vyuo viwili tena dabo dabo kwenye Wilaya yetu, Tunajua neno moja, Watoto wetu walikuwa wakitaka kwenda High school ilikuwa lazima waende nje ya Wilaya, Mama ametuletea High school, tunajua neno moja kuwa Bukombe ilivyokuwa na ilivyo leo ni tofauti, Mbingu na ardhi.
“Tumekubaliana tarehe 29 shughuli zote tunaahirisha, tukupigie kura ili tuendelee kufaidi upendo wako.”- Dkt. Doto Biteko, Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe Mkoani Geita na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akimuombea Kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Viwanja vya shule ya Msingi Ushirombo Wilayani Bukombe leo Jumapili Oktoba 12, 2025.