Home LOCAL DKT.SAMIA KUUNGURUMA JIJINI MWANZA LEO KUNADI ILANI YA CCM KWA WANANCHI

DKT.SAMIA KUUNGURUMA JIJINI MWANZA LEO KUNADI ILANI YA CCM KWA WANANCHI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia siku yake ya pili ya Kampeni Mkoani Mwanza, akitarajiwa kuwa na Mkutano mkubwa wa kampeni Jijini Mwanza leo Jumatano Oktoba 08, 2025.

Jana Oktoba 07, Dkt. Samia alianza kampeni zake Mkoani Mwanza kwa kufanya mikutano ya hadhara ya Kampeni kwenye Wilaya za Misungwi, Sengerema na Nyamagana, akisisitiza kuendelea kusimamia kikamilifu maendeleo ya sekta za Kijamii na kiuchumi kwa kuendelea kutoa ruzuku za pembejeo za kilimo, mbolea na chanjo za mifugo pamoja na kuanzisha kongani za Viwanda kila Wilaya ili kuongeza thamani mazao ya uvuvi, kilimo na mifugo katika jitihada za kuongeza tija na uchumi kwa wananchi.

Dkt. Samia anaingia Jiji la Mwanza leo akiwa kifua mbele na mwingi wa ujasiri kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana Jijini humo ikiwemo ujenzi wa Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati, ujenzi wa shule ya Sekondari Kisenga na Bweni la wasichana shule ya Sekondari Buswelu sambamba na kuongeza uzalishaji wa mazao ya uvuvi na ukamilishaji wa daraja la kihistoria na JP Magufuli, lenye urefu wa Kilomita 3 na kuunganisha maeneo ya Kigongo na Busisi.

Ilani anayoinadi Dkt. Samia kando ya mambo mengine imeahidi kuendeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria kwenda Dodoma kupitia Singida, kuunganisha wateja wapya 1600 na mfumo wa majitaka, kununua boti 2 za doria, ukarabati wa uwanja wa ndege Mwanza, ukarabati mkubwa wa kivuko cha MV Chato 1 pamoja na ujenzi wa barabara za Flyover kwenye makutano ya barabara.

Ilani ya Dkt. Samia pia imeahidi kujenga jengo la kisasa la kibiashara, michezo na utamaduni (one stop centre) eneo la Tampere beach, kujenga Makoroboi city park na Igoma Industrial park, kujenga masoko ya Buhongwa ns Nyegezi pamoja na kuendeleza ukanda maalumu wa kiuchumi Mwanza sambamba na kujenga wodi 12 na majengo 4 ya kuhifadhia maiti kwenye Vituo vya afya Jijiji Mwanza, kujenga nyumba 30 za watumishi wa Vituo vya afya, kukamilisha jengo la wodi ya wazazi, wodi ya upasuaji pamoja na jengo la maabara na jengo la mionzi kwenye Zahanati za Mhandu na Mahina.