Home LOCAL DKT.SAMIA ATOA ELIMU YA UPIGAJI KURA KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA

DKT.SAMIA ATOA ELIMU YA UPIGAJI KURA KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan akionesha mfano wa karatasi ya kupigia kura kwa wananchi wa Buchosa na Sengerema Mkoani Mwanza leo Jumanne Oktoba 07, 2025 katika muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Karatasi halisi yenye kufanana na mfano huo ndiyo itakayotumika siku ya upigaji kura siku ya Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ambapo juu kabisa ndipo lilipo jina la Chama Cha Mapinduzi, Jina la Mgombea wake Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mgombea mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi sambamba na picha zao ambapo alama yako ya tiki upande wa kulia mwa picha zao ndio uthibitisho wa kura yako katika kuwapa ridhaa ya kuunda serikali itakayoongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.

Pembeni ya Dkt. Samia ni Katibu wa NEC, Itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Kenani Laban Kihongosi. Mfano huo wa karatasi za kupigia kura imetolewa kwa Vyama vyote vya siasa ili kutumika kama sehemu ya kutoa elimu kwa wapigakura ili kutokufanya makosa kwenye chumba cha upigaji wa kura.