Home BUSINESS DKT. SAMIA AAHIDI KUIMARISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO NA TEHAMA VIJIJINI

DKT. SAMIA AAHIDI KUIMARISHA HUDUMA ZA MAWASILIANO NA TEHAMA VIJIJINI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Ilani ya Chama chake anayoinadi sasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 imemtaka kuimarisha mawasiliano Vijijini pamoja na kukuza matumizi ya TEHAMA kama sehemu muhimu ya kufikia maendeleo.

Dkt. Samia amebainisha hayo leo Jumamosi Oktoba 04, 2025 wakati wa Mkutano wake mkubwa wa Kampeni kwenye Viwanja vya CCM Sabasaba, Babati Mjini Mkoani Manyara, ikiwa ni siku yake ya pili na ya mwisho ya Kampeni hizo, akihitimisha Kampeni zake kwenye Mikoa ya Kaskazini.

Dkt. Samia amebainisha pia mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta hiyo kwa awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya sita akisema wameongeza upatikanaji wa huduma za simu za kiganjani kutoka asilimia 83 hadi 93 ikitokana na ujenzi wa ujenzi wa minara ya simu 5 kwa Wilaya ya Hanang, 17 Simanjiro pamoja na minara 21 kwenye Wilaya ya Kiteto.