
Mwanasiasa mkongwe nchini, Anna Abdallah amesifu uwezo wa kiuongozi wa Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel John Nchimbi akisimulia namna alivyofuata hatua za baba yake na kuanza uongozi akiwa kijana ndani ya chama hicho.
Bi. Anna ameyasema hayo Oktoba 25, wakati wa kampeni za Dkt. Nchimbi katika eneo la Nansio, Ukerewe, Mwanza.
“Ndugu Nchimbi ameanza akiwa chipukizi wa Chama Cha Mapinduzi, baba yake alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wakati yeye akiwa kijana. Kwa hiyo, amekuzwa ndani ya chama hiki,” amesema.
Kadhalika ameeleza kuwa Dkt. Nchimbi amewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa kipindi hicho Bi. Anna akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake.
Bi. Anna ambaye ni mke wa Spika Mstaafu wa Tanzania, Pius Msekwa amemalizia hotuba yake kwa kumwombea Dkt. Samia, Dkt. Nchimbi na wagombea wa CCM kura za ndiyo katika uchaguzi wa Oktoba 29.




