
Timu ya Wananchi Yanga SC imeibuka kidedeo kwa kuichapatimu ya wekundu wa msimbazi Simba SC bao 1-0, katika mchezo wa Ngao ya Jamii, uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Goli la Yanga SC limefungwa na kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Pacome Zouzou katika dakika ya 55 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.
Mchezo wa Ngao ya Jamii, unaashiria kufunguliwa kwa pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/26, itakayoanza kutimua vumbi Septemba 17, mwaka huu.




