Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM, ameeleza kuwa ikiwa Chama hicho kitapewa ridhaa Oktoba, 29, 2025, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar, zitaendelea kushirikiana pamoja katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Dkt. Samia amebainisha hayo leo Jumamosi Septemba 20, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni Chake Chake Pemba kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale, akisema Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kwa vitendo kutekeleza kaulimbiu yake ya mwaka huu ya “Kazi na Utu, tunasonga mbele”
“Tunafanya kazi ili kuinua Taifa na utu wa mtu na ndio maana tunasema Kazi na Utu, tunasonga mbele, sasa hii ni kwa Taifa hata mtu mmoja mmoja, ukifanya kazi ipasavyo unainua utu wako mwenyewe kwasababu kazi itakulipa ujira na ujira utatumia kufanya maendeleo yako binafsi, lakini ukifunga mikono tu basi utu kidogo unakuwa na wasiwasi.” Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Samia ameainisha kuwa kazi ya Chama Cha Mapinduzi mara zote ni kufikiria kuhusu changamoto za wananchi na kufuatilia yanayolalamikiwa na baadae kuyachukua na kuyafanyia kazi ili kuendelea kustawisha na kuimarisha utu wa Mtanzania.
http://TUTAWAJIBIKA KUSTAWISHA NA KUIMARISHA UTU WA MTANZANIA- DKT. SAMIA