Home SPORTS SIMBA SC YAMALIZANA RASMI NA KOCHA FADLU DAVIDS

SIMBA SC YAMALIZANA RASMI NA KOCHA FADLU DAVIDS

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Uongozi wa klabu ya Simba SC umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Mkuu Fadlu Davids baada ya kuhudumu na timu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa leo septemba 22, 2025, inaeleza kuwa makubaliano hayo ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu.

“Klabu ya Simba inamshukuru Kocha Fadlu kwa kuiongoza Simba kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumalizia nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya NBC”

Aidha, uongozi wa klabu umemtakia kheri na baraka kocha Fadlu katika maisha yake ya soka nje Simba.

Imetolewa na:

Uongozi Klabu ya Simba  22 Septemba, 2025