Home LOCAL MGOMBEA UDIWANI KATA YA LIGANGA JIMBO LA PERAMIHO KUPITIA CHAUMA ATIMKIA CCM

MGOMBEA UDIWANI KATA YA LIGANGA JIMBO LA PERAMIHO KUPITIA CHAUMA ATIMKIA CCM

Katika hali iliyowashangaza wananchi wengi, mgombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Liganga, wilaya ya Songea Vijijini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) Bw. Fulco Komba ameibukia kwenye kampeni za mgombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Peramiho Jenista Mhagama na kuonyesha kuvutiwa kwake na sera nzuri za Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Tukio hilo limetokea Septemba 27, 2025 katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kijiji cha Liganga wakati Bi. Mhagama akinadi Sera za CCM kupitia ilani ya uchaguzi 2025 – 2030.

Hali kadhalika katika tukio lingine lililotokea kwenye mkutano huo, kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bw. Mahmoud Juma amevutiwa pia na sera nzuri za CCM kupitia ilani ya uchaguzi ya 2025 – 2030 na kuamua kujiunga na CCM.

Bi. Mhagama anafanya kampeni za kijiji kwa kijiji katika kata zote za Jimbo la Peramiho katika wilaya ya Songea Vijijini kunadi sera za CCM na kuomba ridhaa ya wananchi kukipigia kura za ndio CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.