Home BUSINESS DKT.SAMIA: TUMEELEKEZA KUANZISHA RANCHI, MASHAMBA YA MALISHO NA MACHINJIO YA KISIASA...

DKT.SAMIA: TUMEELEKEZA KUANZISHA RANCHI, MASHAMBA YA MALISHO NA MACHINJIO YA KISIASA KALIUA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

_Kukamilisha ujenzi hospitali y Wilaya Kaliua 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa ndani ya miaka mitano ijayo ikiwa Watanzania watamchagua kuongoza tena serikali kwa miaka mitano ijayo ataanzisha ranchi na shamba la malisho na uhamilishaji pamoja na ujenzi wa mnada na machinjio ya kisasa kwenye eneo la Kasungu Wilayani humo.

Dkt. Samia ameyaeleza hayo Alhamisi Septemba 11, 2025 wakati wa mkutano wake wa kampeni za uchaguzi Mkuu Wilayani Kaliua Mkoani Tabora, akiahidi pia kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kaliua kwa kujenga majengo mbalimbali ikiwemo jengo la afya ya Mama na mtoto ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi.

“Nami niwahakikishie miaka mitano ijayo hayo sio mambo makubwa sana kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi, tutakwenda kuyafanya kwa ukamilifu wake na kuna maombi nimeyapata kwa Wabunge wenu kwamba ruzuku za mbolea na pembejeo ziendelee, nataka kuwahakikishia kuwa ruzuku kwa pembejeo na mbolea kwa mazao yote ikiwemo tumbaku zitaendelea.” Ameongeza kusema Dkt. Samia.

Mgombea Urais huyo kadhalika ameahidi kufanyia kazi maombi ya wananchi na Wagombea Ubunge wa Majimbo ya Wilaya hiyo ya Kaliua kupitia Chama Cha Mapinduzi ikiwemo ujenzi wa barabara ya Kahama- Tabora na barabara ya Kahama- Ulyankulu kwa kiwango cha lami pamoja na barabara nyingine za ndani kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani humo.