Home BUSINESS DKT. SAMIA KUWAKOPESHA VIJANA BOTI MAALUM ZA UVUVI RUVUMA

DKT. SAMIA KUWAKOPESHA VIJANA BOTI MAALUM ZA UVUVI RUVUMA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Nyasa Mkoani Ruvuma leo Jumapili Septemba 21, 2025 amewaahidi wananchi kuwa amejipanga kuongeza ufugaji wa samaki kwenye vizimba kwa lengo la kuongeza uzalishaji na fursa za ajira jaa Vijana wa Nyasa na Mkoa wa Ruvuma.

Dkt. Samia pia ameahidi kuendelea kutoa vifaa vya kisasa vya uvuvi ikiwemo ukodishaji wa boti maalumu za uvuvi kwa Vijana wa Wilaya ya Nyasa Mkoani humo, kama sehemu ya utekelezaji wa adhma yake na ahadi ya Chama Cha Mapinduzi katika kuhakikisha kuwa anazalisha fursa zaidi za ajira pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Wakati wa Mkutano wake wa Kampeni, siku ya kwanza akiwa Mkoani Ruvuma akitokea Visiwani Zanzibar, Dkt. Samia pia ameahidi kuwa ikiwa atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu wa Jumatano ya Oktoba 29, 2025 ataweka boti maalumu ya uokozi kwenye Ziwa Nyasa ili kutoa huduma za dharura kwa watumiaji wa ziwa hilo muhimu kwa uvuvi na shughuli nyingine za kiuchumi