
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuufanya mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha Biashara, katika ukanda wa ziwa Tanganyika.
Dkt. Samia ametoa ahadi hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata ya Kalinzi, iliyopo katika Wilaya ya Kigoma Vijijini, tarehe 13 Septemba, 2025, akiendelea na kampeni za kuomba kura katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.
“Ahadi yetu kwa Kalinzi na Kigoma kwa ujumla, mkitupa ridhaa kuongoza serikali lengo letu ni kuifanya Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwenye Ukanda huu na ndio maana tunafanya ukarabati wa reli ya zamani, tunaleta reli ya kasi na tunaiunganisha na nchi jirani ili biashara zifanyike kutoka Kigoma Kwenda nchi jirani.
“Lakini tunajua ili hayo yafanyike lazima Vijana na watoto wetu na wananchi kwa ujumla wawe na afya ya kutosha ili waweze kulima na kuzalisha kwa kiasi cha kutosha, lakini wawe na elimu ya kutosha ili waweze kujua wanachokifanya lakini pia kuwe na umeme ili kuwe na usalama, tuweze kufanya kazi zetu kwa usalama, Maji safi na salama- Hii ndio ahadi yetu kwenu wana Kalinzi.” Amesema Dkt.





