Home LOCAL DKT. SAMIA AAHIDI VITUO KUMI VIPYA VYA AFYA IKUNGI MKOANI SINGIDA

DKT. SAMIA AAHIDI VITUO KUMI VIPYA VYA AFYA IKUNGI MKOANI SINGIDA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

“Vijiji vyote vya Wilaya hii 101 vina umeme na tunaendelea na kazi ya kuunganisha Vitongoji. Mbele tunakokwenda mkitupa ridhaa tunakwenda kumaliza kazi yote Tanzania nzima kila mtu awe na umeme lakini pia kwenye afya mbali na kazi tuliyoifanya tunajipanga kujenga vituo vingine kumi vya afya ndani ya Wilaya hii, Vituo 5 kwa Ikungi Mashariki ambavyo vitakwenda kwenye maeneo ya Siuyu, Ligwa, Mkiwa, Isuna na Mang’onyi na vituo vingine vitano kwa Ikungi Magharibi ambavyo vitakwenda Puma, Muntiri, Minyuge, Igongwe na Mwaru.”

Kwa upande wa elimu mbali na yaliyofanyika tutaendelea na sera yetu ya elimu bila malipo pamoja na kuendelea kuongeza miundombinu ya madarasa ya shule za msingi na sekondari hapa Ikungi lakini zaidi ya hapo tumejipanga kujenga chuo cha Ufundi ndani ya Wilaya hii.” – Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza na wananchi wa Ikungi Mkoani Singida leo Jumanne Septemba 09, 2025