Home LOCAL DKT. SAMIA AAHIDI KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME, MAJI NA AFYA MBINGA MJINI

DKT. SAMIA AAHIDI KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME, MAJI NA AFYA MBINGA MJINI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kukamilisha miradi yote ya umeme na Maji Mkoani Ruvuma sambamba na kukamilisha usambazaji wa Umeme kwenye Vitongoji na Mitaa yote nchini ndani ya miaka mitano ijayo.

Akizungumza na maelfu ya wapiga kura na wananchi wa Mbinga Mjini Mkoani Ruvuma leo Jumapili Septemba 21, 2025, Dkt. Samia amesema kwasasa serikali tayari imeshafikisha umeme kwenye Vijiji vyote nchini pmoja na kwenye nusu ya Vitongoji vilivyopo nchini, lengo likiwa ni kuharakisha na kusisimua shughuli za kiuchumi.

Aidha Dkt. Samia amesema kwa Mbinga serikali ya awamu ya sita inaendelea na utekelezaji wa miradi 21 ya uzalishaji maji kwenye maeneo ya Vijijini pamoja na mradi mkubwa wa maji Mbinga Mjini, mradi wenye kugharimu takribani shilingi Bilioni 4. 6, ukitarajiwa kuhudumia Kata 8 za Mbinga Mjini na kumaliza changamoto ya Maji kwenye eneo hilo.