Home LOCAL MSAMA: TUWAUNGE  MKONO WALIOTEULIWA KUGOMBEA 

MSAMA: TUWAUNGE  MKONO WALIOTEULIWA KUGOMBEA 

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

“Ulishakuwa Kiongozi,  sasa ameteuliwa mwingine unanuna nini, kuwa na shukrani,  muunge mkono”

Dar es Salaam 

Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Ndugu Alex Msama ambaye pia alitia nia Ubunge Jimbo la Ukonga ameonesha kushangazwa na baadhi ya watia nia wenzake wanaokasirika kisa tu hawajateuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM kugombea Ubunge.

Msama amewataka Watia nia wote ambao hawajateuliwa kupokea matokeo hayo kwa mikono miwili, kuridhia na kuwaunga mkono wale Walioteuliwa ili Chama chama chao kipate ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 2025.

Aidha, amesema anawashangaa zaidi ambao tayari walishakuwa Wabunge kwa muda wa miaka mitano, kumi, kumi na tano na kuendelea nao wakilalamika badala ya kushukuru Chama na Wananchi kwa kumuamini katika kipindi hicho cha uongozi wake na sasa mtu huyo anapaswa kumuunga mkono mtu mpya maana uongozi ni kama mbio za kijiti, ukichoka unamwachia mwingine.

“Na hapa natamani wote tuinge mfano wa January Makamba, alikuwa na cheo kikubwa lakini jina lake halijarudi na amepokea kwa mikono miwili na kutoa kauli zenye kuendelea kujenga chama, hata mimi pia jina langu halikurudi lakini Nimepokea namuunga mkono mwenzangu Jerry Silaa hiyo ndiyo siasa, tusiwe Wapinzani ndani ya Chama chetu” amesema.