
“Ndugu Watanzania, Kumekuwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya majukwaa ya kijamii zikidai kwamba mimi, Alex Msama, nimejiunga na chama cha Chauma na kwamba ninatarajia kugombea ubunge wa Jimbo la Ukonga kupitia chama hicho.
“Napenda kuwataarifu kwa uwazi na msimamo thabiti kwamba taarifa hizo ni za uongo, hazina msingi wowote, na ni uzushi wenye nia ovu ya kunichafua kisiasa na kijamii.
“Mimi ni mwanachama mwaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sijawahi kufikiria, kuwaza, wala kupanga kuhama CCM. Historia yangu binafsi, imani yangu ya kisiasa, na mchango wangu katika chama hiki ni sehemu ya maisha yangu na misingi ninayoisimamia.
“Nawaomba Watanzania wote wapuuze taarifa hizo za kupotosha, na waendelee kuwa na imani na uongozi wa CCM pamoja na dhamira yangu ya kukitumikia kwa uadilifu na uzalendo chama changu CCM.
“Aidha, nitachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya mtu au kikundi kilichosambaza taarifa hizo za uongo. Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Kifungu cha 16, mtu yeyote anayechapisha au kusambaza taarifa za uongo kwa nia ya kumchafua mtu au kumharibia sifa anatenda kosa la jinai, na anaweza kuadhibiwa kwa faini, kifungo, au vyote kwa pamoja.
“Naendelea kusimama imara na chama changu—CCM—na dhamira yangu ya kuwatumikia Watanzania kwa moyo wa dhati kupitia CCM kwa njia yoyote”
Imetolewa na: Alex Msama
Dar es Salaam, Tanzania
27 Agosti 2025




