
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dkt. Baghayo Saqware, akizungumza katika kikao kazi kati ya Jukwaa la Wahariri na mamlaka hiyo. kilichofanyika leo Agosti 18, 2025 Jijini Dar es Salaam, chini ya usimamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina,

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akzungumza wakati wa salamu za ukaribisho katika kikao kazi hicho.
Na: Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania, (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware, amesema kuwa Mpango wa Bima ya Afya kwa wote una manufaa makubwa kwa watanzania, nakwamba unakwenda kuwaletea unafuu mkubwa na uhakika wa kupata matibabu kwa wakati.
Dkt. Sagware ameyasema hayo katika kikao kazi kati ya Mamalaka hiyo na Wahariri na waandishi wa Habari kilichofanyika leo Agosti 18, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa kufanikiwa kwa mpango huo kunaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha kila mtanzania anapata matibabu ya uhakika wakati wote.
Aidha, amesema gharama ya mpango huo bado haujatajwa ni kiasi gani cha fedha, lakini itatangazwa na Waziri mwenye dhamana hapo baadaye, huku akitangaza fursa kwa watanzania wanaohitaji kuwa mawakala wa Mpango wa Bima ya afya, nakusema kuwa milango ipo wazi kwani vigezo na masharti yake ni nafuu sana.
“Ili kuwa Wakala tembelea tovuti ya https://tiramis.tira.go.tz vigezo na masharti vipo pale. Hivyo natoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa hii ya kiuchumi” amesema.
Akielezea mafanikio ya TIRA Dkt. Saqware amesema, wanufaika wa huduma za Bima nchini wameongezeka kutoka milioni 14 mwaka 2021 hadi milioni 25.9, mwaka huu, huku hamasa ikiendelea ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika.
Pia, amesema mali na mitaji katika soko la Bima imeongezeka kutoka shilingi trilioni 1.2 mwaka 2021 hadi trilioni 2.3,mwaka huu.





