Home BUSINESS MIPANGO YETU MIAKA MITANO IJAYO NI KUONGEZA KASI YA HUDUMA NCHI NZIMA...

MIPANGO YETU MIAKA MITANO IJAYO NI KUONGEZA KASI YA HUDUMA NCHI NZIMA – SANGWE 

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na Mwandishi Maalum

SELF Microfinance imejivunia hatua za mafanikio iliyopata ndani ya kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa mipango yake [2021 – 2025].

Ndani ya kipindi hicho Mfuko huo ulio chini ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha umeweza kuongeza mtaji wake kutoa TZS Bil. 58.47 hadi kufikia TZS 59 Bil.

Umeweza kuhudumia wananchi ambao wengi ni wajasiriamali wadogo kupata mikopo nafuu na kukuza mitaji ya biashara zao, kujikomboa ki-uchumi.

Sasa unaongeza uwezo wake kwa kuweka mikakati madhubuti zaidi ambayo itachochea kasi ya kupanua huduma zake, kuwafikia wananchi hasa wajasiriamali wadogo, wengi nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa SELF Microfinance Santili Yona amesema hayo wakati alipozungumza mbele ya waandishi wa habari, akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Paul Sangawe.

Pamoja na mkutano huo na waandishi wa habari, Sangawe ambaye ni awamu ya pili kuteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza tena bodi hiyo alikuwa pia anakutana na wajumbe wake.

“Hiki ni kikao cha kueleza SELF Microfinance tulipotoka, tulipo na tunapoelekea,” amesema CEO Santieli.

Amebainisha Mfuko huo una jukumu kubwa kwanza kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali pia kutoa mikopo kwa taasisi za fedha ambazo zinalenga kutoa huduma hiyo ngazi ya chini kwa jamii.

Amebainisha “Kwa kipindi cha 2021 hadi 2025 tumeweza kutoa mikopo ya TZS 199.9 Bil. na wananchi 183,381 wamenufaika,”.

CEO Santaeli amesema wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wanawajengea uwezo wajasiriamali ki-biashara.

“Tangu tumeanza 2015 hadi sasa, tumefanikiwa kutoa mikopo zaidi ya TZS 397 Bil. tumewafikia wanufaika 183,381 na 53% ni wakina mama,” amesema.

Amebainisha wanatoa huduma hiyo ya mikopo nafuu kwa kwa watu mbalimbali moja wamejikita kwenye biashara, kilimo pamoja na taasisi hizo zinazopesha.

“Tumejipanga vizuri, kuhakikisha tunafikia malengo yetu na malengo ya Serikali,” amesisitiza.

Mwenyekiti wa Bodi Paul Sangawe amesema ‘kiu’ yake kubwa ni kuona wanafikia malengo wanayojiwekea, malengo ya Kitaifa na Kimataifa pia.

“Mtaji wa mfuko umeongezeka, kukua kwa mtaji ni pamoja na uwezo wa mfuko kuweza kutekeleza majukumu ya mfuko ambayo tumepewa,” amesema.

Ameongeza “Utoaji wa mkopo zaidi ya TZS 199.9Bil. hizi ni fedha nyingi ukiangalia kwa biashara kubwa kubwa unaweza kusema fedha hizi si nyingi sana.

“Lakini kwa wafanyabiashara ndogo ndogo fedha hizi ni nyingi sana. Ukizigawa ambazo zinaweza zikabadilisha maisha ya wananchi wngi kujiendeleza katika shughuli za uchumi na kuongeza kipato.

“Hili ni jukumu mojawapo ambalo tumepewa, tungependa kuongeza wanufaika zaidi, matawi pia ili tusogeze huduma zetu karibu zaidi na wananchi,” amesema.

Mfuko huo unatoa huduma nchi nzima, hata hivyo kwa sasa una matawi yake Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Iringa, Kahama, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Tanga pamoja na Zanzibar.