Home LOCAL MGOMBEA UBUNGE CCM KAFITI WILLIAM AUNGANA KUTAZAMA UZINDUZI KWA NJIA YA TELEVISHENI._MWANZA.

MGOMBEA UBUNGE CCM KAFITI WILLIAM AUNGANA KUTAZAMA UZINDUZI KWA NJIA YA TELEVISHENI._MWANZA.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. *Kafiti William Kafiti*, ameungana na viongozi wa chama, wanachama na wananchi wa Manispaa ya Ilemela kushuhudia uzinduzi wa kampeni za CCM kwa njia ya televisheni leo, Agosti 28, 2025, katika viwanja vya Furahisha, Jijini Mwanza.http://MGOMBEA UBUNGE CCM KAFITI WILLIAM AUNGANA KUTAZAMA UZINDUZI KWA NJIA YA TELEVISHENI._MWANZA.

Tukio hilo la kitaifa lilifanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers, mkoani Dar es Salaam, na kuongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maelfu ya wananchi wa Ilemela na Jiji la Mwanza walijitokeza kushiriki, wakionesha mshikamano na kuunga mkono dhamira ya CCM ya kuendeleza maendeleo ya Taifa.