Home BUSINESS MFUKO WA SELF WATOA MIKOPO YA SH. BILIONI 196.9 KWA WATANZANIA

MFUKO WA SELF WATOA MIKOPO YA SH. BILIONI 196.9 KWA WATANZANIA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na: Mwandishi wetu,  DAR ES SALAAM 

Serikali kupitia Mfuko wa SELF, imetoa Jumla ya Shilingi Bilioni 196.9 zilizowanufaisha zaidi ya watanzania 183,000 katika kipindi cha miaka minne cha uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo uliopo Chini ya Wizara ya Fedha, Bi. Santiel Yona, katika wa Kikao kazi kati yao na Wahariri na waandishi wahabari, kilichofanyika Agosti 15, 2025, Jijini Dar es Salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR).

Bi. Yona ameeleza kuwa kuanzia mwaka 2021 hadi June 2025, SELF imeweza kuwafikia wanufaika Zaidi ya 183,000, ambapo katika idadi hiyo, wanawake wakiwa 97,000, na wanaume ni 86,000.

“Mfuko huu ambao upo Chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umekuwa ukihakikisha utoaji wa mikopo ni salama kwa wanufaika ukizingatia masharti nafuu ili kuwafikia wanufaika wengi zaidi hasa wananchi wa kawaida”

“Sisi kazi yetu kubwa ni kuwapa watu fursa za kufanya shughuli za uzalishaji mali, na hili ni jukumu letu muhimu la kuhakikisha Watanzania wanaendelea na shughuli zao bila vikwazo” amesema Bi Santiel.

Aidha amesema kuwa Mfuko huo unatoa mikopo kwa masharti nafuu kulingana na miongozo iliyopo, nakwamba wamekuwa wakitoa ushirikiano wa karibu kwa mnufaika, pindi anapopatwa changamoto ya kuchelewesha kufanya marejesho yake kabla ya kuchukua hatua za adhabu.

Pia, Mfuko huo umejielekeza katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhakikisha Watanzania wanatumia Nishati safi ya kupikia, kwa kutoa mikopo kwa wananchi. wakishirikiana na wadau mbalimbali wanaosambaza majiko yanayotumia Nishati hiyo katika mkoa wa Dar es Salaam.