Home LOCAL MAJINA WAGOMBEA UBUNGE CCM HADHARANI AGOSTI 23

MAJINA WAGOMBEA UBUNGE CCM HADHARANI AGOSTI 23

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kutoa taarifa kuhusu ratiba ya vikao vya kitaifa vya Chama, vitakavyofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika tarehe 21 Agosti 2025, kikifuatiwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC).Taifa kitakachofanyika tarehe 23 Agosti 2025.

Aidha, ajenda ya vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa; Wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.

Vikao vyote vitafanyika jijini Dodoma.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

CPA Amos Gabriel Makalla
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO
17 Agosti 2025.