
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imetoshana nguvu na Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa 0-0 katika mchezo wake wa mwisho wa kundi A ya michuano ya CHAN inayoendelea nchini, kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.
Mchezo huo umepigwa katika Dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam, ambapo umeshuhudiwa na maelfu ya watanzania waliofurika katika uwanja huo kuipa nguvu timu yao.
Tanzania inasubiri mshindi wa mchezo wa Kenya na Zambia, na Morocco na DRC itakayochezwa Agosti 17, ili kujua timu itakayocheza nayo.




