
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kitafanyika tarehe 19/7/2025 saa 4:00 asubuhi Jijini Dodoma,
Taarifa iliyotolewa leo Julai 15, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, imeeleza kuwa Kikao hicho kitatanguliwa na kikao cha Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, inayoendelea kuketi Jijini humo kwa ajili ya kupokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wa Jimbo na Viti Maalum.
Aidha kikao hicho, ni sehemu ya maandalizi ya agenda za Kikao cha Kamati Kuu.





